Jumatatu, 24 Oktoba 2016



W
akala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)         umejipanga                kuhakikisha    kwamba unaboresha huduma zake ili ziweze kuendana na gharama  wanazotozwa  wadau  kwaajili  ya    huduma
husika kwa mujibu wa kanuni na sheria za tozo hizo.

OSHA ilianzishwa August 31,  2001  chini  ya  Sheria ya Wakala Na. 30 ya mwaka 1997 kwaminajili ya koboresha hali ya afya na usalama wa wafanyakazi wawapo kazini na majukumu yake makubwa ni pamoja na kusajili sehemu za kazi, kufanya kaguzi za Afya na Usalama mahali pa kazi, kufanya uchunguzi wa afya  za wafanyakazi katika sehemu za kazi, kufanya mapitio ya tathmini za athari za kiafya na kiusalama sehemu za kazi na kutoa leseni ya kukidhi matakwa ya Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi.
Majukumu mengine ni kuhakiki ramani na michoro ya sehemu za kazi, kutoa mafunzo ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi, kutoa elimu kwa umma juu ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kutoa ushauri wa kitaalam kuhusiana na masuala ya Afya na Usalama Mahali    pa Kazi na kufanya uchunguzi wa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
Kutokana na umuhimu wa majukuma ya OSHA katika jamii, Wakala umelenga kuboresha zaidi mifumo ya utendaji kazi wake na hatimaye kuweza kufikia lengo  la kuanzishwa kwake ambalo ni kuhahakisha kwamba sehemu za kazi zinakuwa salama wakati wote.