|
husika kwa
mujibu wa kanuni na sheria za tozo hizo.
OSHA ilianzishwa August 31,
2001 chini ya Sheria ya Wakala
Na. 30 ya mwaka 1997 kwaminajili ya koboresha hali ya afya na usalama wa
wafanyakazi wawapo kazini na majukumu yake makubwa ni pamoja na kusajili sehemu
za kazi, kufanya kaguzi za Afya na Usalama
mahali pa kazi, kufanya uchunguzi wa afya
za wafanyakazi katika sehemu za kazi, kufanya mapitio ya tathmini za athari za kiafya na kiusalama sehemu za kazi na kutoa leseni ya kukidhi
matakwa ya Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa
Kazi.
Majukumu mengine ni kuhakiki ramani na michoro ya sehemu za kazi, kutoa
mafunzo ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi, kutoa elimu kwa umma juu ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kutoa
ushauri wa kitaalam kuhusiana na
masuala ya Afya na Usalama Mahali pa
Kazi na kufanya uchunguzi wa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
Kutokana na umuhimu wa majukuma ya OSHA katika jamii, Wakala umelenga kuboresha zaidi mifumo ya utendaji
kazi wake na hatimaye kuweza kufikia lengo
la kuanzishwa kwake ambalo ni kuhahakisha kwamba sehemu za kazi zinakuwa
salama wakati wote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni